FURSA KWA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA ZA UDHIBITI WA VIUMBE HAI WAHARIBIFU

TANGAZO


 

Mkurugenzi wa kituo cha utafiti na udhibiti wa viumbe hai waharibifu (SUA Pest Management Centre) kilichopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro, anawatangazia kuwa kituo kinatoa fursa ya wabunifu wa Teknolojia mbalimbali za udhibiti wa viumbe hai waharibifu kuonana na watafiti wake.


Teknolojia inayokidhi vigezo, itafanyiwa majaribio ya Kisayansi kwa lengo la kuhakiki ufanisi,kuboresha na kuunganishwa na wenye viwanda.
 

Zoezi hili litaanza kuanzia tarehe 1 / 12/ 2019 hadi tarehe 30 /1/2020.
 

Mhusika anatakiwa awe na Teknolojia bunifu ya kudhibiti viumbe hai waharibifu kama vile Panya, Mende,  Kunguni, Viroboto,  Mbu, Dumuzi  n.k
 

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nao sasa kwa anuani zifuatazo;
Simu: 0623-125990
Tovuti: www.spmc.sua.ac.tz

 

Share this page