Kituo cha Taarifa za Kilimo - SUA kina lengo la kuunganisha chuo na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo kwa kuwapatia taarifa sahihi zinazohusiana na kilimo, mifugo, misitu, maendeleo vijijini na nyanja nyingine. Wakulima na wadau wengine watapata taarifa hizi kwa kuingia kwenye Ghala la Machapisho ya Ugani (SUAOR) au kuwasiliana na kituo cha Taarifa za Kilimo - SUA.