Kongamano la Tiba Asili SUA

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kimeahidi kufanya kazi bega kwa bega na wadau mbalimbali waliopo katika Mnyororo wa Thamani wa Bidhaa za Tiba Asili kwaajili ya kuibua Bunifu na kupata suluhisho la Kisayansi kuhusu changamoto zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa biashara ya bidhaa za Mimea Dawa nchini.

Kongamano la Tiba Asili SUA

Hayo yamebainishwa siku ya Jumatatu Agosti 29, 2022 na Mkurugenzi wa Uzamili, Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Profesa Esron Karimuribo wakati akimuwakilisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma na Tafiti Profesa Maulid Mwatawala ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Kwanza la Kisayansi la Tiba Asili Tanzania la siku mbili lililofanyika SUA Kampasi Kuu ya Edward Moringe Sokoine.

Endelea kusoma habari hii: https://www.conas.sua.ac.tz/chemistryphysics/news/kongamano-la-tiba-asili-sua

Share this page