Wananchi wa Arusha Wapongeza Menejimenti ya SUA kwa Kuwawezesha Kiuchumi Kupitia Msitu Wake wa Mafunzo wa Olmotonyi

Wananchi wanaoishi kandokando ya Msitu wa Mafunzo wa Olmotonyi Mkoani Arusha wamekishukuru Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kuwapatia nafasi ya kupata Kuni za kupikia pamoja na maeneo ya kilimo hivyo kusaidia kupata kipato cha kuendesha maisha yao na familia zao kwa miaka mingi.

Wananchi wa Arusha Wapongeza Menejimenti ya SUA kwa Kuwawezesha Kiuchumi Kupitia Msitu Wake wa Mafunzo wa Olmotonyi

Wananchi wakitoka na kuni kwenye msitu unaovunwa.

 

Shukrani hizo zimetolewa na Wananchi hao wakati wakiongea na Waandishi wa habari ndani ya msitu huo unaomilikiwa na SUA ambao ni maalumu kwa ajili ya Mafunzo kwa Vitendo kwa wanafunzi wanaosoma Shahada mbalimbali za Misitu katika Chuo hicho.

Akizungumza wakati akipata Kuni za kupikia kwenye eneo ambalo linavunwa mbao kwa sasa Bi. Mami Lowasa amesema toka azaliwe amekuta wazazi wake wakiingia kwenye msitu huo wa Olmotonyi  kulima kwenye maeneo ambayo uongozi wa Kituo hicho umekuwa ukiruhusu kufanyika kwa shughuli za kilimo.

Bi. Mami Lowasa akizungumza na Waandishi wa habari (Hawapo pichani) kwenye Msitu wa Mafunzo wa Olmotonyi wakati akikata kuni.

Bi. Mami Lowasa akizungumza na Waandishi wa habari (Hawapo pichani) kwenye Msitu wa Mafunzo wa Olmotonyi wakati akikata kuni.

Ukiangalia katika mji huu wa Arusha wananchi wengi wa hali ya chini na kati wanategemea kilimo kuendesha maisha yao lakini maeneo ya kilimo ni machache sana lakini mahusiano mazuri ya SUA na Jamii yamewezesha wananchi wengi kupata maeneo ya kulima mazao mbalimbali hasa mahindi, maharage na mboga ndani ya msitu huu kwenye maeneo ya wazi yaliyovunwa mbao na yenye miti midogomidogo iliyopandwa",  Alieleza Bi. Mami.

Kwa upande wake Mwananchi mwingine Julias Sumayaki Baada ya wazazi wake wote wawili kufariki aliachiwa wadogo zake watatu kuwatunza na kuwasomesha lakini hana kazi wala shamba ambalo anaweza kulima kutosheleza mahitaji yake na familia hiyo aliyoachiwa na wazazi wake.

Sina neno zuri la shukrani ninaloweza kulisema kueleza furaha na shukrani zangu kwa uongozi wa SUA kutokana na msaada mkubwa tunaoupata baada ya kuturuhusu kupata kuni kwenye mabaki ya miti ambayo imevunwa, Msitu huu sisi ndio maisha yetu mimi na wadogo zangu lakini na vijana wengi hapa mjini    alisema bwana Sumayaki.

Aliongeza kupitia msitu huu nimeweza kupata kuni za kutumia nyumbani na wadogo zangu lakini pia zingine kwenda kuuza Arusha mjini na kupata fedha ambazo zimeniwezesha kusomesha wadogo zangu nilioachiwa na wazazi wangu lakini pia kupata mahitaji yangu pale pale nyumbani, kwa kweli huu msitu ni mkombozi kwetu.

Akizungumzia mchango huo wa Msitu wa Olmotonyi Meneja wa Kituo cha Mafunzo cha Msitu huo Bwana Said Kiparu amesema pamoja na kutoa nafasi kwa jamii inayozunguka msitu huo kupata kuni na maeneo ya Kilimo lakini Wananchi hao wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali za majangili wa msitu.

Meneja wa Kituo cha Mafunzo cha Msitu huo Bwana Said Kiparu akizungumza na Waandishi wa habari kituoni hapo kuangalia kazi zinazofanywa na kituo hicho katika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa SUA.

Meneja wa Kituo cha Mafunzo cha Msitu huo Bwana Said Kiparu akizungumza na Waandishi wa habari kituoni hapo kuangalia kazi zinazofanywa na kituo hicho katika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa SUA.

Jamii inaona faida ya uwepo wa msitu huu na wanauona kuwa ni wa kwao kwa kuwa tunawaruhusu kukata kuni hasa matawi kwenye maeneo ambayo tumevuna magogo ya mbao lakini pia tunapomaliza kuvuna wakati tunapanda miti mingine wao tunawapa nafasi ya kulima mazao madogo madogo hususani viazi mviringo na mboga miti ikiwa midogo na wao wanashiriki kuitunza wanapohudumia mazao yao alifafanua Bwana Kiparu.

Naye Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Dkt. Agnes Sirima amesema kuwapa Wananchi wanaozunguka Msitu wa Olmotonyi fursa ya kupata kuni na kulima ni mchango  mzuri unaotolewa na Chuo kwa jamii kama majirani wanaozunguka msitu huo.

Kwa namna hii ndio tunajenga mahusiano mema na jamii inayotuzunguka na kuwafanya wajifunze masuala ya umuhimu wa utunzaji misitu lakini pia kuwa walinzi wazuri wa msitu na hivyo kupunguza changamoto za uchomaji moto tofauti na ilivyo nyanda za juu kusini ambako majanga ya moto huaribu sana misitu mingi ya kupandwa na kuleta hasara kwa wahusika alieleza Dkt. Sirima.

Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Dkt. Agnes Sirima CKatikati) akizungumza na Waandishi wa habari je ya msitu huo na kushoto kwake ni Afisa Mawasiliano na Masoko wa SUA BI, Suzana Magobeko.

Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Dkt. Agnes Sirima (Katikati) akizungumza na Waandishi wa habari je ya msitu huo na kushoto kwake ni Afisa Mawasiliano na Masoko wa SUA Bi, Suzana Magobeko.

Rasi huyo wa Ndaki amesema pamoja na kupata faida hizo lakini pia baadhi ya jamii inayozunguka msitu zimepata ajira na wengine hufanya vibarua mbalimbali ambavyo hupata fedha za kuendesha maisha yao huku wakijifunza pia hatua zote za upandaji, utunzaji, uvunaji na uchakataji wa magogo ya miti na kupata mbao.

Kibao cha kuingia kwenye msitu wa mafunzo wa Olmotonyi

Kibao cha kuonesha unapoanzia Msitu wa mafunzo wa Olmotonyi 

 

 

 

Share this page