ZALISHENI VIAZI LISHE KUWAINUA KIUCHUMI NA KUWALETEA AFYA BORA-ERNEST MKONGO

 

Bwana Mkongoa lisema siku zote watafiti hufanya tafitikatika mambo mbalimbali lakini kwaasa watafiti hao wamekuja na mbinu mpya ya kuwatumia wanafunzi wa shule za msingi kuwa walimu kwa jamii wanazotoka baada ya watafiti hao kuona kuwa mbinu hiyo inauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kwenye mbinu ya ugani.

Ameongeza kuwa muitikio wa kutosha waliouonyesha wazazi nikiashiria tosha kwake kuwa mbinu ya kuwatumia watoto imeweza kuleta mafanikio makubwa katika kufikisha elimu kwajamii.

Aidha amewaasa vijana walioko mashuleni kutumia vema elimu waipatayo kwani itawasaidia kuwaingizia kipato wawapo shuleni na baada ya masomo yao nakuboresha lishe yao kwa kula viazi hivyo

Pia Makongo alisema wale watu wanaodhani shughuli za kilimo ni adhabu waache dhana hiyo kwani ukifuta kanuni bora za kilimo hasa kwa zao la viazilisheli utapata faida kubwa zitakazokuwesha kupambana na umaskini

Vilevile amewaondoa hofu wanafunzi na walimu wa shule ya Kigugu iliyopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kwa kuwahimiza walime zao hilo kwa wingi na kuwa ofisi yake itakuwa tayari kuwaletea mashine ya kuwasaidia kukata viazi kwa kuwarahisishia kazi na kuwapunguzia muda wa kufanya kazi hiyo na hivyo wataweza kutengeneza bidhaa hiyo kwa kuuza viazi na unga wake lakini pia watapata pesa kwa kukodisha mashine hizo