Na:Alfred Lukonge

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi stadi Prof. Joyce Ndalichako amefanya ziara katika shule ya Sekondari ya Utete na kuwatia moyo walimu wa shule hiyo kufanya kazi kwa bidii ingawa wanafanya kazi katika mazingira magumu.

 Akiwa ziarani kwenye shule hiyo iliyopo tarafa ya Utete wilayani Rufiji mkoa wa  Pwani Prof. Ndalichako alipata fursa kutembelea nyumba za walimu pamoja na mabweni ya wavulana na wasichana ambapo alishuhudia miundo mbinu mibovu hasa ya vyoo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                  

Na: Latifa Kassim

Vijana waishio   eneo la Mafisa katika Manispaa ya Morogoro wanatarajia kunufaika na mradi wa kilimo ambao umelenga kuwapatia ardhi pamoja na vitendea kazi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na SUAMEDIA  Mwenyekiti wa chama cha kilimo cha mbogomboga eneo la Mafisa Bw. Dotto Magomba amesema kuwa pamoja na kunufaika na mradi huo, pia ametoa wito kwa vijana kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuepuka makundi yasiyofaa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     

Picha na mtandao  

             

Na:Vedasto George

Wakazi wa Kata ya Lukobe katika Manispaa ya  Morogoro,  wameiomba serikali   kutunga  sheria ya kudumu kwa wazazi na walezi wenye tabia ya  kutelekeza   watoto wanaozaliwa na ulemavu katika familia zao.

Wakizungumza na SUAMEDIA kwa nyakati tofauti Bi. Ashura Mkapale, Bw Lazaro Joseph, na Bi. Zaituni Williamu  wamebainisha kuwa  wazazi  hususani wanaume wamekuwa  na tabia ya kuwakimbia  wake zao pindi  wanapojifungua watoto wenye ulemavu hali  inayowawia vigumu kwenye malezi ya watoto hao.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA