Na:Farida Mkongwe

Meya wa manispaa ya Morogoro Mh. Paschal Kihanga amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa elimu hapa nchini na hivyo kuamua kutoa msaada wa madawati kwa shule ya msingi Mkundi.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 70 yaliyotolewa na Chama cha Wanataaluma wa SUA  (SUASA) ambapo amewataka wadau wengine hasa wazawa wa kata hiyo ya Mkundi kuhakikisha wanajitoa kwa hali na mali katika kuisaidia shule hiyo.

 

Akizungumza katika hafla hiyo Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema SUA imedhamiria kuunga mkono jitihada za Rais za kuboresha elimu na kuongeza kuwa kazi itakuwa ngumu kwa SUA katika suala zima la ufundishaji iwapo wanafunzi watakuwa hawajaandiliwa vizuri kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na ndiyo maana wanafanya jitihada za makusudi katika uboreshaji wa elimu ya msingi.

TOA MAONI YAKO HAPA