Na: Catherine Mangula Ogessa

 

Jamii imetakiwa kuelewa kuwa mabadiliko ya tabianchi yamechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ukame hivyo hawanabudi kulinda vyanzo vya maji ili kuondokana na ukame unao jitokeza katika maeneo mengi.

 

Kauli hiyo imetolewa na mhadhiri mwandamizi kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA Prof. Henry Mahoo wa Idara ya Uhandisi Kilimo wakati akiongea na SUAMEDIA.

 

 

 

Prof. Mahoo amesema kuwa jamii hainabudi kuelewa kuwa hivi sasa kuna hali ya ukame imeongezeka  tofauti na kipindi cha nyuma ambapo kulikuwa na maji mengi lakini kwa sasa uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji, ikiwemo uchomaji misitu inayo zunguka vyanzo vya maji na maeneo mengine vimekuwa ni vyanzo vya ukame huo.

 

Ameongeza kuwa jamii ni vyema ikalinda vyanzo vya maji kwa kuhifadhi ili kuondokana na ukame ambao kwa sasa umekuwa ni tishio na imefika mahali inaonekana kama ni kitu cha kawaida kwa kila mwaka kuona watu wakichoma misitu na wengine kufanya shughuli za uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji.

 

Aidha amezitaka pia mamlaka zinazo husika na udhibiti wa uaharibifu wa mazingira kuhakikisha inatumia dhamana hiyo waliyopewa kwa kuhakikisha wanawachukulia hatua za kisheria wale wote wanaohusika na uchomaji wa misitu.

 

 

 

 

TOA MAONI YAKO HAPA