Na: Catherine Mangula Ogessa

Jamii imetakiwa kuwa na desturi ya kujipanga mapema na suala la uvunaji wa maji ya mvua ili pindi mvua zinapo anza waweze kuvuna maji kwa wingi kwa lengo la kukabiliana na shida ya maji wakati wa ukame.

Kauli hiyo imetolewa na mhadhiri mwandamizi kutoka idara ya uhandisi kilimo wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Henry Mahoo wakati akiongelea misingi ya uvunaji maji ya mvua.

Mmoja wa wataalamu wa uvunaji maji akitoa maelekezo ya jinsi gani ya kuvuna maji hayo(Picha na mtandao)                              

Prof. Mahoo Amefafanua kuwa ni muhimu kutambua wastani wa mahitaji ya maji unayo yahitaji, kuangalia endapo una paa linaloweza kuvuna kiasi hicho cha maji unayoyahitaji, lakini pia uwe na mfumbi pamoja na bomba za kupelekea maji.

TOA MAONI YAKO HAPA