Na: Godfrey Mahanda

Mtu mmoja aliye fahamika kwa jina la Emmanueli Mwanchale dereva wa pikipiki maarufu kama boda boda amenusurika kifo baada ya kupata ajari mbaya iliyotokea jana majira ya jioni hapa mjini morogoro.

Akizungumza na SUAMEDIA Bw, Ally Mngurumi shuhuda wa ajali amesema  chanzo cha ajali ni kulikwepa roli la mafuta lililokuwa likitokea  dar es salaam kuelekea dodoma  huku akiendesha pikipiki hiyo kwa mwendo kasi na  kusababisha kutumbukia mtaroni.

 

                                                                                                       Picha na mtandao.

Aidha tabia ya kuendesha vyombo hivyo bila kuzingatia sheria za  usalama barabarani imekuwa chanzo kikubwa cha ajali  nyingi katika manispaa ya Morogoro na hivyo kupelekea kupata vilema na vifo.  

TOA MAONI YAKO HAPA