Na:Kizito Ugulumo

Wito umetolewa kwa akina mama wajawazito kote nchini kujitokeza kuwa na tabia ya kwenda kliniki na kupima afya zao ikiwemo kujua maendeleo ya mtoto aliye tumboni ili yafanyike maandalizi ya kitaalamu yatakayopelekea uzazi salama  

Akizungumza na SUAMEDIA  Prof.Andrea Pembe kutoka Chuo Kikuu cha Afya,Tiba na Sayansi Muhimbili amesema kuwa  vifo vya  mama mjamzito pamoja na mtoto  vinaweza kuepukika kama watafuata maelekezo mbalimbali wanayopewa wakienda kliniki.

           

                                                                                                    Picha na mtandao.

Wataalamu na wadau wa afya wapo mjini Morogoro kujadili namna ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga  kanda ya mashariki mkutano unaoratibiwa na ofisi ya mkuu katika mkoa wa Morogoro. 

 

TOA MAONI YAKO HAPA