Na:Mwandishi Wetu

Imeelezwa kuwa maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi hapa nchini usababishwa zaidi na utumiaji wa Dawa ya Kulevya hususani kwa njia ya kujidunga sindano jambo linalopelekea kupoteza nguvu kazi kwenye jamii na kuathiri taifa.  

Akizungumza na SUAMEDIA Dr.Tumwesige Tayomba amesema kuwa matumizi ya Dawa ya Kulevya ni janga linaloathiri zaidi vijana wenye wastani wa miaka 15-30 hivyo lisipotiliwa mkazo litakuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.

 

                                                                                        Picha na mtandao.

Pia Dr.Tayomba ametoa wito kwa mashirika yanayopambana na Dawa hizo kuipa weledi jamii juu ya madhara ya matumizi ya dawa hizo.  

Aidha Dr. Tayomba ameongeza kuwa kinga ya msingi ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya imo ndani ya familia ambyo iweze kumkubali muathirika ili aweze kuachana na kilevi kwa kumpa huduma nzuri bila ya kumnyanyapaa. 

Vilevile Dr.Tayomba amebainisha kuwa mwarubaini wa kuacha dawa hizo uanzie kwenye ngazi ya familia kwa wazazi kuwalea watoto kwenye maadili pamoja na yule anayetumia dawa hizo apewe ushirikiano wa kutosha ili aweze kuacha.

 

TOA MAONI YAKO HAPA