Na:Alfred Lukonge

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA upande wa taaluma Prof. Peter Gillah amesema kuwa tathimini ya kina inatakiwa kufanyika kwenye uchimbaji wa maji yaliyo chini ya ardhi ili uchimbaji huo usiweze kuleta athari kwa vyanzo vingine vya maji vilivyopo juu ya ardhi.

Prof. Gillah amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye muendelezo wa mradi wa Groundwater Futures in Sub-Saharan Africa ( GROFUTURES ) mradi uliojikita kufanya tathimini ni namna gani ya uchimbaji wa maji yaliyopo ardhini  chuoni SUA mapema leo.

Aidha Prof. Gillah amebainisha kuwa kupitia mradi huo tathimini ya kina itafanyika kugundua kuna kiasi gani cha maji ardhini ili yapate kutobolewa kwa matumizi salama ya binadamu na kwenye kilimo pia, ili kuondokana na umaskini.

Kwa upande wake mkuu wa timu ya utafiti wa mradi huo nchini Tanzania Prof. Japhet Kashaigila amesema kuwa uchimbaji wa maji ya ardhini kiholela umeathiri kwa kiasi kikubwa nchi ya Pakistan kwa ardhi , nyumba  na barabara zake kupasuka  kutokana na presha ya maji hayo kutoka chini kubadilika.

Pamoja na hayo Prof. Kashaigila pia amebainisha kuwa mradi huo utakuwa ni wa miaka minne na utahusisha mataifa matano ya Afrika na matatu kutoka nchi za ulaya.

TOA MAONI YAKO HAPA