Na:Vedasto George

Kaimu Jaji mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma  anatarajia  kupokea orodha ya majina ya Mahakimu na Majaji  ambao wanadaiwa kuvuruga kesi  za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na  uuzaji na uvutaji wa dawa za kulevya.

Hayo  yamesemwa hapo jana na kamishina wa mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya nchini Bw.Rogers William Siyaga  wakati wa mkutano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na waandishi  wa habari ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaamu Bw.Paul Makonda  kwa ajili ya kupambana na dawa za kulevya.

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye hivi karibuni anatarajia kupokea orodha ya majaji wenzake waliovuruga kesi zinazohusiana na dawa za kulevya.(Picha na mtandao)

Kwa upande wake mkuu wa  mkoa wa Dar es salaamu Bw.Paul Makonda amekabidhi orodha ya majina 97 ya watu  wanaojiusisha na dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto umewashwa dhidi ya watu  wanaofanya biashara hiyo haramu .

TOA MAONI YAKO HAPA