Na:Daileth .I. Mbele

Bw. Chirau Ali Mwakwere ambaye amekuwa balozi wa Kenya akiiwakilisha nchi ya Tanzania amejiuzulu wadhifa huo ambapo Mwanasiasa huyo mkongwe ametangaza uamuzi huo ili agombee ugavana wa kaunti ya Kwale.

Mwanasiasa huyo mkongwe ambaye kati ya kipindi cha mwaka 2004 na 2005 amewahi kuwa waziri wa Mambo ya Nje na baadaye waziri wa Uchukuzi wa Kenya, ametangaza pia kuhamia chama cha Upinzani ODM akitokea Muungano wa Jubilee ambao ulishinda uchaguzi wa mwaka 2013.

 

                                                    Picha na mtandao.

Uchaguzi mkuu nchini Kenya unatarajiwa kufanyika mwezi wa nane mwaka huu, viongozi wote wa Umma wanaotaka kugombea nafasi za kisiasa wanalazimika kujiuzulu nafasi zao kabla ya Februari 15 mwaka huu.

TOA MAONI YAKO HAPA