Na:Nasma Hamisi

Bei za mazao ya nafaka katika mikoa mbalimbali nchini zimeonesha kupanda kwa kiasi kidogo ukilinganisha na bei za wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa mtandao wa kufuatilia tathmini ya bei za mazao nchini uitwao NINAYO, bei ya mchele kwa Manispaa ya Dodoma, kilo moja ya mchele imeuzwa kwa shilingi 1600 huku ikionekana kupanda katika soko manispaa ya Iringa ambapo mchele kilo moja umeuzwa shilingi 1950.

 

                                                                                                                                    Picha na mtandao.

Aidha kwa upande wa soko la Iringa kilo moja ya mahindi imeuzwa kwa shilingi 1,900 ambapo imepanda kwa ongezeko la shs mia nne ukilinganisha na bei ya kilo moja ya mahindi siku ya Jumatano machi 15 ambapo iliuzwa kwa shilingi 1500.

Hata hivyo kwa upande wa vitunguu tani 1 ya vitunguu kwa mkoa wa Dodoma, kwa leo machi 17 imeuzwa kwa shilingi 65,000 ikilinganishwa na siku ya tarehe 16 machi ambapo tani 1 ya vitunguu kwa mkoa humo Dodoma, iliuzwa kwa shilingi 14,300.

TOA MAONI YAKO HAPA