Na:Catherine Mangula Ogessa

Clouds FM imethibitisha ukweli wa habari na picha zilizokuwa zimeenea katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa mkuu wa mkoa wa Dar s salaam Paul Makonda  alivamia kituo hicho majira ya usiku akiwa na askari waliokuwa na silaha.

Akiongea na Redio hiyo mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media  Bw. Ruge Mutahaba amethibitisha kufika kwa mkuu huyo wa mkoa wa Dar Es Salaam katika studio hizo na kuwa kilichowashitua ni mazingira aliyofika nayo katika studio hizo.

 

Picha na mtandao.

 

Wakati huo huo Waziri wa habari utamaduni na michezo Mhe. Nape Nauye amewasili asubuhi hii katika kituo cha utangazaji cha Clouds jijini Dar es salaam.

TOA MAONI YAKO HAPA