Na:Kizito Ugulumo

Wanawake mkoa wa Morogoro wametakiwa kutumia vyema mikopo wanayoipata kupitia vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa huku wakijikita zaidi katika shughuli za uzalishaji mali ili waweze kujitafutia kipato na maendeleo katika maisha yao ya kila siku

Akizungumza na SUAFM Bi, Judith Mbaga mwanakikundi kutoka mfuko huo wa VICOBA Mazimbu amesema kumekuwa na kasumbua kwa baadhi ya kinamama kukopa fedha hizo na kuzitumia katika matumizi mengine yasiyokuwa ya uzalishaji mali na kuwapa shida baadhi yao katika urejeshaji mikopo hiyo. 

 

 

Aidha Bi. Mbaga  amewaomba viongozi wa vikundi hivyo kote nchini kutohifadhi katika sanduku kiasi kikubwa cha fedha na badala yake wazipeleke benki kuepuka upotevu wa fedha ambao umekuwa ukijitokeza kwa vikundi vingi kabla ya kuvunja vikoba vyao 

TOA MAONI YAKO HAPA