Na:Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali maalum.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Bw. Hamza Johari imebainisha  kuwa kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.

Image result for drones

                                                                                             Picha na mtandao.

 

 Aidha taarifa hiyo pia imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

TOA MAONI YAKO HAPA