Na:Bujaga Izengo Kadago

Hifadhi ya taifa ya Serengeti nchini Tanzania imetajwa kama kivutio cha 16 kwa ubora duniani ikiwa ndio kivutio pekee kutoka Afrika kati ya vivutio 30 bora duniani mwaka huu wa utalii.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Marekani linaloratibu safari za kitalii duniani, ambapo limeielezea hifadhi ya Serengeti kuwa inavivutio vya misafara ya mamilioni ya wanyama na ndege wanaosafiri toka pande moja ya hifadhi kwenda pande nyingine wakati wa mazalio na wakati wa kutafuta malisho.

Image result for serengeti national park main gate

                                                                                                  Picha na mtandao.

Miongoni mwa wanyama walioelezwa na shirika hilo la utalii duniani kuwa watalii watawashuhudia kwa makundi makubwa ni pamoja na pundamilia, swala, nyani na fisi wenye mabakamabaka.

Kivutio cha kwanza duniani kwa mujibu wa shirika hilo la safari za watalii duniani ni jiji la Roma nchini Italia likifuatiwa na jiji la Sydney Australia na kivutio cha tatu ni jiji la Porto nchini Ureno na kivutio cha 30 ambacho ni cha mwisho katika orodha hiyo ni mji wa St. Lucia kutoka Carribeani Marekani ya kati.

Daraja lililokaguliwa wiki mbili zilizopita na rais Uhuru Kenyata wa Kenya na kuelezwa kuwa ni muarubaini wa kutengwa kwa eneo la Busia kulikofanywa na serikali zilizopita, limevunjika kabla hata halijamalizika kujengwa.

Tukio hilo linaloelezwa kuwa ni aibu kwa serikali ya sasa ya Kenya kwani ilikuwa ikitumia ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali kama daraja hilo kujinadi katika wakati huu wa uchaguzi mkuu nchini Kenya.

 

Hadi sasa sababu za kuvunjika kwa daraja hilo hazijafahamika na kampuni iliyokuwa ikijenga daraja hilo kampuni kutoka Uchina haijaeleza lolote kuhusu sababu za kuvunjika kwa daraja hilo lililokuwa linaunganisha sehemu nyingine za Kenya na mkoa wa Busia.

TOA MAONI YAKO HAPA