Na:Kizito Ugulumo

WANANCHI wa  kata ya  Nyanzwa  wilaya ya  Kilolo mkoa  wa  Iringa  wamemwomba mbunge wa  jimbo la Kilolo  Venance Mwamoto kumwomba  Rais  Dkt John Magufuli kufika  katika  kata  hiyo  ili  waweze kumwona  na  kumpongeza kwa  kazi nzuri anayoifanya ya  kupambana na  vita  ya uchumi   katika Taifa . 

Wakizungumza jana wakati wa  mkutano  wa mbunge wao  Venance Mwamoto  wamesema Kuwa wao kama  wananchi  wa kata ya  Nyanzwa  wamekuwa  wakifuatilia  kazi na  utendaji  wa  Mheshimiwa  Rais Magufuli   hasa kuyatekeleza  kwa  vitendo yale  yote  aliyoahidi  wakati wa kampeni na hivyo wana hamu kubwa ya kuzungumza naye katika wilaya yao. 

Image result for magufuli                                                                                                                      Picha na mtandao.

Aidha  wananchi hao  wamesema  kero  yao kubwa katika kata  hiyo ambayo  wananchi wake  wanaishi kwa  kutegemea  kilimo cha  umwagiliaji ni  kupata  bwawa  la  kuendeshea  kilimo   hicho,  huku  wakimpongeza mbunge  wao  kwa  kutekeleza ahadi yake ya  mawasiliano ya  simu kama  alivyoahidi  wakati wa kampeni. 

 

TOA MAONI YAKO HAPA