Picha na mtandao

 

LIVERPOOL KUIKARIBISHA LEEDS KOMBE LA LIGI HII LEO

Na:Ayoub Mwigune 

Klabu ya Liverpool ipo nyumbani hii leo kucheza dhidi ya Leeds katika michuano ya ligi ya shirikisho la soka Uingereza na tayari meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kwamba mchezaji wake toka Brazil Philipe Coutinho ataikosa mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi.

 

Meneja huyo amesema kwamba coutinho anatarajiwa kurejea  uwanjani mwezi januari 2017  na tayari meneja huyo amesema ataziba pengo la coutinho kwa kumpanga Young lad Ben.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

   

 

Picha na mtandao

 

ULIMWENGU KUTIMKIA ULAYA

Na: Adam Ramadhan

Mshambuliaji  wa  timu  ya  Taifa  ya  Tanzania  Thomas  Ulimwengu  amekiri kwenda  kuanza  maisha  mapya  ya Soka barani  Ulaya  baada  mkataba  wake  wa  kuitumikia klabu  ya  TP Mazembe  ya  Congo DRC  kumalizika.

 

Licha  ya  klabu  ya  TP Mazembe  kutaka  kumuongezea  mkataba  mshambuliaji  huyo  hakuwa  tayari  na sasa  akili  yake  yote  ameielekeza  Ulaya,  huku akisema kuwa tayari  vilabu kadhaa  vimeanza  kumuhitaji  japo  hakutaka  kuviweka  hadharani.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

     
 

ST.MARY’S  YAPONGEZWA                           

Na:Ayoub Mwigune na Halima Katala

Afisa michezo mkoa wa morogoro Neema Msithar  ameupongeza uongozi wa shule ya St.Marys mkoani Morogoro kwa kuwa na utaratibu wa kuandaa siku ya michezo ambayo inawashirikisha wazazi pamoja na walimu kwani siku hiyo imekuwa ni nyenzo ya kujenga uhusiano mzuri kati ya walimu pamoja na wazazi .

 

Akizungumza kwa niaba ya Afisa huyo wa michezo   mkoa, Afisa elimu wa manispaa ya Morogoro  bi. Imakulata Fungo alisema kuwa michezo inatakiwa ipewe kipaumbele kwani inachangia sana katika kuufanya mwili  uwe na afya njema na kuongeza uwezo wa kufikiri pia aliomba walimu wa michezo kuendelea kuwafundisha watoto michezo mbalimbali kwani kufanya hivyo kutawajengea wanafunzi hali ya kupenda shule.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

Picha na matandao

 

MAMELODI SUNDOWNS YATWAA UBINGWA WA AFRIKA

Na: Adam Ramadhan

Klabu   ya  Mamelodi  Sundowns   wametangazwa   na  shirikisho  la  soka  Afrika  (CAF)  kuwa  mabingwa  wapya wa  Afrika  kwa  ngazi   za  vilabu  mwaka  2016  baada   ya  kuifunga  na   kufungwa   katika  michezo  miwili  ya  fainali   ya  mashindano  hayo  dhidi  ya  Zamaleki.

 

Mchezo   wa  mkondo   wa kwanza   wa  fainali  hizo  ulichezwa  katika  mji   wa Atteridgeville  Afrika  ya  Kusini  ambapo  Mamelodi  Sundowns  waliibuka  na  ushindi  wa  magoli  3-0 dhidi ya  wageni  wao  Zamaleki, katika  mkondo   wa  pili  hapo   jana  jumapili Mamelodi   Sundowns  wakafungwa   1-0  dhidi  ya  wenyeji  wao  Zamaleki.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

Picha na mtandao

 

CHELSEA YAIADHIBU MAN U

Na: Adam Ramadhan

Klabu   ya  Chelsea  jana Jumapili 23 mwezi huu imeiadhibu  kipigo  kikubwa  cha jumla  ya  magoli 4-0 klabu  ya  Manchester  United  katika  mchezo   wa   ligi  kuu   ya  nchini  England, mchezo   uliofanyika  katika  uwanja  wa  Stamford  Bridge .

 

Mchezo  huo  ulimrejesha kocha  aliyetimuliwa  msimu  uliopita  Jose Mourinho wa Chelsea   lakini   kwa  sasa  akiwa  ni  mkufunzi   wa  Manchester  United  na   kuambulia   kipigo   kikubwa  kikiwa  ni kipigo  kikubwa  zaidi kukipata  tangu  alipofungwa  na  Barcelona  magoli   5-0  Novemba  2010  katika  La  liga.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

                                                                     

Picha na mtandao

 

Man U YAINYUKA FENEBARCE 4-1

Na: Adam Ramadhan

Michuano   ya  Ligi  ndogo   ya  mabingwa  barani   Ulaya  imeendelea  tena  usiku   wa  kuamkia  leo  ambapo michezo  mbalimbali  imepigwa  katika  viwanja  tofauti  huku  Paul  Pogba  aking’ara  na  timu  yake  ya  Manchester  united.

 

Manchester   United   wakiwa  katika  uwanja   wa  Nyumbani   wameweza  kuibuka  na  ushindi   wa  goli  4-1  dhidi  ya  Fenebarce  na  kujiweka  katika  mazingira  mazuri  katika kundi  A   huku  Feyernod  wakiifunga  Zorya  goli  1-0.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

     

                                                                

                  PICHA NA MTANDAO

 

AZAM FC YACHEZEA KICHAPO

Na:Ayoub Mwigune     

       
Ligi kuu ya Vodacom iliendelea hapo jana kwa michezo mbalimbali ambayo ilichezwa katika viwanja tofauti ambapo katika mji wa Shinyanga Stand united waliweza kuiadhibu klabu ya Azam fc kwa 1-0 na kuwafanya kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma kwa alama moja nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba SC.


Jijini Mbeya klabu ya Mbeya City ilishindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa vinara wa ligi hiyo Simba sc ambapo safu ya ushambuliaji ya Simba ikiongozwa na Kichuya na Ajibu ilionekana kuwa mwiba mbele ya safu ya ulinzi ya klabu hiyo ya Mbeya city.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     

                                                                                    Picha na mtandao

 

NYERERE CUP KUENDELEA LEO

Na: Adam Ramadhan


Mashindano ya soka  ya  Nyerere   Cup   yaliyoanza  wiki   iliyopita  mkoani  Morogoro  yataendelea  tena  leo  kwa  kuwakutanisha  mafahari  wawili  kutoka  kihonda  Mlunda FC na  Topsite FC  katika  uwanja  wa  sabasaba majira  ya  saa 10:00  alasiri.


Hapo  jana  michuano  hiyo  iliendelea  ambapo  Chamwino  market FC  walitolewa  kwa  penati  na  timu  ya  Mwere  FC  kufuatia  sare   ya   jumla  magoli  2-2  katika  dakika  90.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

   

                                                                          

 

 SWANSEA YATIMUA KOCHA

Na: Adam Ramadhan

Klabu   ya    Swansea   city   imemfuta   kazi    kocha   wake   Fransesco   Gudolini  kutokana  na  mwenendo   mbaya   wa  klabu   hiyo   katika  ligi   kuu   ya   Uingereza   na   nafasi   yake   kuchukuliwa  na  Bod  Bradley.

Kocha   huyo   amefukuzwa  baada  ya  timu  yake   kupata   alama  nne   katika   michezo   saba   ya  ligi  hiyo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

                                                                       

 

 

SAMMATA HATARI ZAIDI DAKIKA  20 ZA MWISHO

Na:Adam  Ramadhan 

Mshambuliaji Mbwana Samatta kutoka Tanzania  anayeichezea  klabu  ya  KRC Genk  ya Ubelgiji  tayari  amefikisha  mabao sita ukijumlisha yale ya Ligi Kuu ya Ubelgiji pamoja na michezo ya ligi ya  Europa.

 

Sammata  amefunga mabao hayo sita, mawili ni ya Europa na manne ni ya ligi lakini inaonekana  Samatta ni hatari zaidi katika dakika za mwisho hasa  akiingia  wakati  wa  mabadiliko.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 


 

 

 

 

 

 

                                                   

 

 MO BEJAIA YAJINASIBU KUBEBA UBINGWA

 

Na: Adam Ramadhan

Mchezo  wa   fainali  wa  kombe  la  shirikisho  utazikutanisha  klabu  za  MO Bejaia ya Algeria na TP Mazembe ya DRC  ambapo  itapigwa  mechi ya ugenini na nyumbani katika fainali inayozikutanisha timu zilizotoka kundi moja katika michuano ya makundi.

Mohamed  Sabah  ni  moja  ya  wanakamati   wa  benchi  la  ufundi  la  klabu  ya  MO Bejaia  amesema  kuwa  kwa  sasa  klabu  ipo   vizuri   na  wanamatumaini  makubwa  ya  kufanya  vyema  watakapokutana  na  mabingwa   watetezi  wa  kombe  hilo klabu  ya   TP Mazembe.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     

Picha na mtandao

 

KILIMANJARO QUEEN FAINALI LEO CHALENJI

 

Na: Adam Ramadhan

Timu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, leo inatarajiwa kuvaana na Kenya katika mchezo wa fainali wa Kombe la Chalenji kwenye Uwanja wa Ufundi uliopo Njeru, mjini Jinja huko nchini Uganda.

Timu hiyo ya Bara ilitinga fainali baada ya kuwatoa wenyeji Uganda katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki, ikishinda 4-1 huku nayo Kenya kwa upande wake ikiitoa Ethiopia katika mchezo mwingine wa nusu   fainali.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     
                                                   

WAFANYAKAZI WA SUA WAHIMIZWA KUSHIRIKI MICHEZO YA IDARA

Na: Adam Ramadhan

Wafanyakazi  wa  chuo  kikuu  cha Sokoine  cha  kilimo (SUA)  wamehimizwa  kujitokeza wingi na  kushiriki   katika  michezo   iliyoandaliwa  na  idara  ya  michezo  ya  chuo  hicho  kwa   mwaka   2016, ambapo  michezo  hiyo  inatarajiwa  kuanza  Septemba  21.

Akizungumza  na  wajumbe  waliohudhuria  kikao   cha  kuandaa  mashindano  hayo  Mwenyekiti   Lwoga  Ladslaus  ambaye  pia  kiongozi   wa  Idara  ya  michezo  chuoni hapo,  amesema  kuwa  michezo  hiyo  itatoa  fursa  ya   kujenga  mahusiano  na  kufanya  afya  kuwa  bora  kwa  washiriki.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     

 

SAVIO YAPANIA KUFANYA MAKUBWA MICHUONI YA KANDA TANO AFRIKA


Na:Alfred Lukonge


Mchezaji nguli ambaye pia ni mkufunzi wa mchezo wa mpira wa kikapu Mohamed Yusufu wa timu ya Savio amesema kuwa ana uhakika na timu yake kuchukua ubingwa wa mashindano ya kanda ya tano ya Afrika yanayotegemewa kuanza Oktoba 1 mpaka 7 katika viwanja vya ndani vya Taifa jijini Dar es Salaam.

" Kwa mazoezi tunayofanya na utimamu wa kila mchezaji siku zinavyokwenda kuelekea mashindano nina imani mwaka huu mwali lazima abaki Tanzania" amebainisha Yusufu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

  

 

     

 

 

 

 

Picha na mtandao
 

 

 WACHEZA SOKA GHALI DUNIANI


Na: Adam Ramadhan

Mchezo   wa  Soka  kwa  sasa  ndio   umekuwa  mchezo  wenye  gharama  zaidi  duniani  hasa  katika  manunuzi  ya  wachezaji, lakini  pia  ndio  mchezo  wenye  mashabiki  wengi  zaidi  ulimwenguni  kwa  sababu  umekuwa  na  mvuto  sana.


SUAMEDIA  inakuletea  orodha  ya  wachezaji   walionunuliwa  kwa  bei  ghali  zaidi  duniani  mpaka  sasa, Paulo  Pogba  amesajiliwa  kutoka  Juventus  kwenda  Manchester  United  kwa  ada paundi  milioni 89 na  kuwa  mchezaji  ghali zaidi  duniani  kwa sasa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     

 

 

MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WA SUA KUANZA SEPTEMBA 12


Na: Adam Ramadhan

Wafanyakazi  wa  chuo  kikuu  cha Sokoine  cha  kilimo (SUA)  wamehimizwa  kujitokeza  na  kushiriki   katika  michezo   iliyoandaliwa  na  idara  ya  michezo  ya  chuo  hicho  kwa   mwaka   2016, ambapo  michezo  hiyo  inatarajiwa  kuanza  Septemba  12.


Akizungumza  na  wajumbe  waliohudhuria  kikao   cha  kuandaa  mashindano  hayo  Mwenyekiti   Lwoga  Ladslaus  ambaye  pia  kiongozi   wa  Idara  ya  michezo  chuoni,  amesema  kuwa  michezo  hiyo  itatoa  fursa  ya   kujenga  mahusiano  na  kufanya  afya  kuwa  bora  kwa  washiriki.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     

 

UHAMIAJI YAIBUKA KIDEDEA

Na: Fadhila Kizigo    

Timu ya Netball  Uhamiaji imeibuka na ushindi katika michuano ya ligi daraja la kwanza iliyofanyika mkoani Morogoro huku  Naibu Waziri wa Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo  Mh. Anastazia Wambura  akitoa wito kwa wanawake kushiriki michezo ya Netball.

Uhamiaji imeibuka kidedea kwa kufunga magoli 776 kati ya michezo kumi waliyocheza na kufanikiwa kuwa mshindi wa michuano hiyo wakifuatiwa na timu ya Polisi Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     

 

 

 HAMOUD AVUTWA KATIKA AKADEMI YA PSG


Na: Adam Ramadhan

Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Ufaransa, PSG umeamua kumvuta katika akademi ya klabu hiyo mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, Haytham Saadun Hamoud mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mzaliwa wa jiji la Dar es Salaam.

Safari yake ya soka ilianzia katika mpango wa kuzalisha vipaji kwa klabu ya Mtibwa Sugar, baada ya hapo alielekea Oman ndipo wasaka vipaji wa PSG walipomuona

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     
 

NGASSA RUKSA KUJIUNGA NA KLABU YOYOTE KABLA YA SEPTEMBA 6

Na: Adam Ramadhan

Baada  ya  Mrisho  Ngassa  kurejea  nchini  akitokea  Afrika  ya  Kusini  kumekuwa  na hali  ya  sintofahamu  kwa  baadhi ya  wadau  wa soka nchini   juu   ya  kujiunga  na  iwapo Ngassa anaweza  kujiunga  na klabu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

 Lakini  Afisa  habari  wa  TFF  Alfred Lucas  amesema  kuwa  Ngasa  anaruhusiwa  kujiunga  na  klabu  yoyote  kabla  ya  Septemba 6 mwaka huu  kabla  ya dirisha  kubwa  la usajili la FIFA  kufungwa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     
         

MICHUANO YA NETBALL LIGI DARAJA LA KWANZA KITAIFA MKOANI MOROGORO.

 Na: Suzane Cheddy

 

Katika michuano ya kitaifa ya netiboli inayoendelea mjini Morogoro, timu ya Polisi Arusha imeibuka na ushindi wa magoli 59 kwa 56 dhidi ya timu ya Tumbaku Morogoro.

Akizungumza na SUA MEDIA mwenyekiti kamati ya ufundi taifa Asha Sapi amesema kuwa michuano imeanza vizuri kutokana na wachezaji wote kuonyesha ushindani katika uchezaji pamoja na nidhamu kwa waamuzi.

  Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save