Picha na mtandao                                               

Na:Calvin Gwabara

Kamati ya Bunge ya Maliasili na mabadiliko ya tabia nchi kutoka nchini Malawi imeipongeza Serikali,Uongozi wa hifadhi za taifa TANAPA na watanzania kwa namna wanavyolinda na kuhifadhi maliasi za taifa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Werani Chirenga walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Mikumi Mkoani Morogoro kwa lengo la kujifunza na kuona namna Tanzania inavyopiga hatua katika kusimamia maliasili za nchi ili na wao wapate mbinu hizo na kuweza kuzitumia katika kutatua changamoto zinazoikabili nchi yao kwenye utunzaji wa maliasili zao.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

      Picha na mtandao                   

Na:Vaileth Samwel

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira  ameongoza mamia ya watanzania kuwapokea watoto Dorene Mshana, Wilson Tarimo na Sadia Ismail katika uwanja wa KIA waliorejea nchini kutoka  Marekani walikokwenda kwa ajili ya matibabu  kutokana na ajali ya gari iliyotokea mei sita mwaka huu na kusababisha vifo vya wanafunzi 32 na walimu 2 na dereva 1 wa shule ya Lucky Vicent ya mkoani Arusha

 Akisoma hotuba kwa niaba ya makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu, Mh. Nghwira amesema kuwa serikali inawashukuru wale wote walifanikisha matibabu ya watoto hao likiwemo shirika la ndege Sumatra purse lililojitolea kuja nchini kwa ajili ya uwokozi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                    

Na:Farida Mkongwe          

Imeelezwa kuwa changamoto kubwa inayowakabili wakulima wengi nchini ni Sehemu kubwa ya udongo unaotumika kwa kilimo kutochanganuliwa na kupimwa hali inayowafanya baadhi ya wakulima kutovuna mazao yenye tija.

Hayo yameelezwa na Mhadhiri na Mtafiti kutoka Ndaki ya Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Dr. Mawazo Shitindi wakati akizungumzia umuhimu wa kupima udongo katika kongamano la wadau wa kilimo biashara ambalo limefanyika mjini Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA