Na:Alfred Lukonge

Imeelezwa kuwa zuio la   watoto wa umri chini ya miaka tisa kupanda pikipiki bila muangalizi linatoka kwenye  sheria ya usafirishaji  inayomtaka mtu yeyote anayetumia chombo hicho kuvaa kofia ngumu ambazo mara nyingi huwa ni kubwa hivyo kushindwa kuwatosha watoto hao.

Hayo yamesemwa na Sajenti Danny Mloli kutoka Ofisi ya Mkuu wa Kituo cha Usalama Barabarani mkoani Morogoro kitengo cha elimu kwa umma alipozungumza kwenye kipindi cha mchakamchaka kinachorushwa hewani na redio SUA FM na kubainisha kuwa mtu anapopanda Pikipiki mwenyewe ndio anatakiwa kukaa vizuri jambo ambalo linakuwa gumu  kwa watoto hao kutokana na umri wao.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

              

Na:Kimaro Rajab.

Vijana mkoani Morogoro na kwingineko wameshauriwa kujitokeza ili kupata mafunzo mbalimbali ya uzalishaji mali yakiwemo mafunzo ya kilimo na ufugaji  kupitia miradi mbalimbali iliyo chini ya shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa (SUMA JKT).

Akizungumza katika viwanja vya maonesho ya 24 ya wakulima nanenane mkoani Morogoro, mmoja wa wakilishi wa shirika hilo Emmanuel Nkina amesema kuwa licha ya mafunzo yatolewayo pia SUMA JKT inatoa mikopo yenye riba nafuu lengo likiwa ni kumuwezesha mtanzania wa kipato cha chini kujikomboa na umaskini.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                

Na:Ilimina Materu

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Taasisi zote za elimu  hapa nchini kutoa mafunzo  ipasavyo ili wanafunzi wapate  elimu sahihi na baadae  kujiajiri wenyewe pamoja na kuleta ushindani kwenye soko la ajira.

Mh. Majaliwa ametoa wito huo hii leo  kwenye ufunguzi wa maonesho ya 12 ya elimu ya juu katika viwanja vya maonesho vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam  na kubainisha kuwa anazishukuru Taasisi za elimu ya juu kwa kuona umuhimu wa maonesho hao jambo litakalopelekea vijana kuwa wabunifu zaidi. 

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA