Image result for Dr. Hassan Mshinda           

 

Na:Bujaga Izengo Kadago

Imeelezwa kuwa azma ya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa viwanda inaweza kufikiwa kwa haraka iwapo taifa litaongeza nguvu katika uwekezaji katika teknolojia.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Dr. Hassan Mshinda alipozungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

     

       Image result for KAIRUKI

Picha na mtandao.

   

 

Na:Kizito Ugulumo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki amesema Watumishi wa  Umma walioghushi vyeti watachukuliwa hatua za kisheria.

Mhe. Kairuki ameyasema hayo katika kikao kazi na watumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke,Tarafa ya Mbagala na kusisitiza kuwa wote  walioghushi vyeti hawapo kazini na wameshafutwa katika orodha ya malipo ya Serikali.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

         

     Image result for magufuli

Picha na mtandao

     

 

Na:Kizito Ugulumo

WANANCHI wa  kata ya  Nyanzwa  wilaya ya  Kilolo mkoa  wa  Iringa  wamemwomba mbunge wa  jimbo la Kilolo  Venance Mwamoto kumwomba  Rais  Dkt John Magufuli kufika  katika  kata  hiyo  ili  waweze kumwona  na  kumpongeza kwa  kazi nzuri anayoifanya ya  kupambana na  vita  ya uchumi   katika Taifa . 

Wakizungumza jana wakati wa  mkutano  wa mbunge wao  Venance Mwamoto  wamesema Kuwa wao kama  wananchi  wa kata ya  Nyanzwa  wamekuwa  wakifuatilia  kazi na  utendaji  wa  Mheshimiwa  Rais Magufuli   hasa kuyatekeleza  kwa  vitendo yale  yote  aliyoahidi  wakati wa kampeni na hivyo wana hamu kubwa ya kuzungumza naye katika wilaya yao. 

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA