Image result for SHULE YA MSINGI

Picha na mtandao

                                                                                  

Na:Salama  Namga-DSJ

Wanafunzi wa darasa la saba katika shule za msingi Mkoani Morogoro  wametakiwa kuongeza juhudi katika masomo yao katika muhula huu wa pili wakati wakijiandaa na kufanya mtihani wa taifa utakaofanyika mwezi wa tisa mwaka huu.

Akizungumza na SUAMEDIA  Mwalimu mkuu wa shule  ya msingi Kiwanja cha Ndege Nivocavit  Monyo amewataka wanafunzi kutobweteka na matokeo mazuri waliyoyapata katika mitihani yao ya kujipima kimkoa ambayo ilionyesha ufaulu mkubwa bali waongeze juhudi katika masomo yao ili waweze kufaulu vizuri zaidi katika mitihani ya mwisho ya kitaifa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

    Picha na mtandao                                     

Na:Kizito Ugulumo

Imeelezwa kuwa watu wengi hapa nchini hususani wanawake, wasichana na watoto wamekuwa wakifanyiwa  vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo ukeketaji, ndoa za utotoni, ubakaji, vipigo na mengineyo lakini wengi wao wamekuwa hawana mahali ya kukimbilia kwa ajili ya  kupata msaada zaidi.

Katika kukabiliana na hali hiyo kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Morogoro  kwa kushirikiana na wamisionari wa YMCA wa  usharika wa Lempaala nchini Finland wamefanikiwa kujenga kituo ambacho kitawahudumia waathiriwa wa vitendo vya ukatili wakati wakisubiri kupata msaada zaidi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                                                  

Na:Alfred Lukonge

Watu kutoka sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi wameonekana kuwa na mwamko mkubwa wa kutaka kulima kilimo bora na cha kisasa kwa kutumia teknolojia zinazopatikana katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.

Hayo yamesemwa na Bujaga Izengo Kadago ambaye ni kiongozi wa SUAMEDIA alipokuwa anatoa tathmini ya jumla ya mwitikio wa watu kwenye kutembelea banda la chuo cha SUA kwenye maonyesho ya 41 ya biashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA